10 MARA
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Mwenye kusema: “Laa ilaaha illallaah, Wahdahuu laa shariyka Lah, Lahul-mulku, walahul-hamdu, wahuwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr”, (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allah tu, Peke Yake, Hana mshirika. Ni wake yeye tu ufalme, na ni zake yeye tu Himdi, na Yeye ni Muweza wa kila kitu” Atakayesema hayo mara kumi anapoamka ataandikiwa mema mia moja, na atafutiwa maovu mia moja, na atapata thawabu sawa na za kumwacha huru mtumwa, na atapewa kinga kwayo kwa mchana huo hadi jioni. Na atakayesema hayo wakati wa jioni atapata mfano wa hivyo’’. Ameipokea Ahmad kwa nambari (8719), na Shekh Ibnibaz, Allah amrehemu, amesema kuwa Isnadi yake (Orodha ya wapokezi wake) ni nzuri.
1 MARA
أَمْسَيْنَا وَأَمْسَى الْمُلْكُ لِلَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هَذِهِ اللَّيْلَةِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا وَشَرِّ مَا فِيهَا، اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْكَسَلِ، وَالْهَرَمِ، وَسُوءِ الْكِبَرِ، وَفِتْنَةِ الدُّنْيَا، وَعَذَابِ الْقَبْرِ
“Amsaynaa wa-amsal-mulku lillaah, walhamdu lillaah. Laa ilaaha illa-llaah, Wahdahuu laa shariyka Lah. Allahumma Innii as-aluka min khayri haadhihil-layla, wakhayri maa fiihaa. Wa-auudhu bika Min-sharrihaa washarri maa fiihaa. Allaahumma innii a’uudhu bika minalkasali, walharami, wasuu-ilkibar, wafitnatid-dun-yaa, wa-adhaabilqabri. (Tupo jioni na ufalme ni wa Allah, na himdi ni za Allah Peke yake, hana mshirika. Ewe Mola wangu, nakuomba kheri zilizomo katika usiku wa leo na kheri za vilivyomo humo. Na ninakuomba kinga dhidi ya shari yake na shari ya vilivyomo humo. Ewe Mola wangu, naomba kinga kwako dhidi ya uvivu, na ukongwe na uzee mbaya, na mtihani wa dunia na adhabu ya kaburini”. Na anapoamka asubuhi aseme kama hivyo: “Asbahnaa wa-asbahal-mulku lillaah, walhamdu lillaah. Laa ilaaha illa-llaah, Wahdahuu laa shariyka Lah. Allahumma Innii as-aluka min khayri haadhalyaum, wakhayri maa baadahuu. Wa-auudhu bika Min-sharrihii Min-sharri maa fii Haadhalyaum Washarrimaa baadah. Allaahumma innii a’uudhu bika minalkasali, walharami, wasuu-ilkibar, wafitnatid-dun-yaa, wa-adhaabilqabri. Imepokewa na Muslim kwa nambari (2723).
1 MARA
اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ خَلَقْتَنِي، وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ
Bwana wa Istighfari (Maneno yenye uzito mkubwa katika kumuomba Allah msamaha): “Allahumma Anta Rabbii, Laa Ilaaha illaaa Anta, Khalaqtanii Wa-Anaa ‘Abduka, WaAnaa ‘Alaa ‘Ahdika Wawa’adika Mastata’tu, A’udhu Bika Min-Sharri Maa Swana’atu, Abu’u Laka Bini’imatika Alayya, Wa-abuu-u Laka Bidhanbii, Fagh’fir Lii Fa-innahuu Laa Yaghfirudh-dhhunuuba illaa Anta”. (Bwana wa Istighfari ni kusema: “Ewe Allaah, Wewe ni Mola wangu, hakuna wa kustahiki kuabudiwa ila wewe tu. Umeniumba, na mimi ni mja Wako. Nami niko katika ahadi yako na agano lako kiasi cha uwezo wangu. Naomba kinga kwako dhidi ya ubaya wa niliyoyafanya. Nakiri neema zako kwangu, na nakiri kukukosea, basi naomba unisamehe, kwa sababu hakuna wa kusamehe dhambi ila wewe tu. Amesema Mtume kuwa: (Atakayesema maneno haya mchana akiwa na yakini nayo, na akafa mchana wake huo kabla ya kuingia jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa Peponi. Na atakayesema maneno haya usiku akiwa na yakini nayo na akafa kabla hajafika asubuhi, basi yeye ni miongoni mwa watu wa Peponi)”. Ameipokea Bukhaari, kwa nambari (6306).
1 MARA
اللَّهُمَّ بِكَ أَمْسَيْنَا وَبِكَ أَصْبَحْنَا وَبِكَ نَحْيَا وَبِكَ نَمُوتُ وَإِلَيْكَ الْمَصِير
Anapopambazukiwa mmoja wenu aseme: “Allahumma Bika Aswbahnaa, Wabika Amsaynaa, Wabika Nahyaa, Wabika Namuut, Waileyikan-nushuur”, (Ewe Allah, kwa sababu yako tumeingia katika asubuhi, na kwa ajili yako tuliingia jioni, na kwa sababu yako tumekuwa hai, na kwa sababu yako tutakufa, na kwako tu tutafufuliwa). Na ikifika jioni aseme: “Allahumma Bika Amsaynaa, Wabika Aswbahnaa Wabika Nahyaa Wabika Namuut, Wailayikal Maswiir”, (Ewe Allah, kwa sababu yako tumefika jioni, na kwa sababu yako tumefika asubuhi, na kwa sababu yako tuko hai na kwa sababu yako tutakufa na marejeo ni kwako tu). Amepokea Hadithi hii Abudaud kwa nambari (5068), Tirmidhiy kwa nambari (3391), Nasaai kwa nambari (9836) {Assunanul Kubraa}, Ibnimaja kwa nambari (3868). Shekh Ibnibaz - Allah amrehemu - amesema kuwa orodha (Isnadi) ya wapokezi wake ni sahihi.
1 MARA
اللَّهُمَّ فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ نَفْسِي وَمِنْ شَرِّ الشَّيْطَانِ وَشِرْكِهِ، وَأَنْ أَقْتَرِفَ عَلَى نَفْسِي سُوءًا، أَوْ أَجُرَّهُ إِلَى مُسْلِمٍ
“Allahumma, Faatwirassamaawaati Wal-ardhwi, ‘Aalimalghaybi Wash-shahaada, Laa ilaaha illaa An’ta, Rabba Kulli Shay-in Wamaliikah, A’uudhu Bika Min-sharri Nafsii, Wamin-sharri Shaitwaani Wa Shirkihii, Wa-an-aqtarifa ‘Alaa Nafsii Suu-an, au Ajurrahuu ilaa Muslim”, (Ewe Allaah, Mjuzi wa Ghaibu (mambo yasiyo onekana kwa macho) na yanayo onekana, hakuna anayestahiki kuabudiwa ila wewe tu, Mola wa kila kitu na Mmiliki wake. Nakuomba kinga dhidi uovu wangu mwenyewe na uovu wa shetani na shirki yake na kujichumia uovu mimi mwenyewe au kumfanyia ubaya Muislamu). Amesema Mtume –SAW-: “Yaseme hayo asubuhi na jioni, na unapolala”. Imepokewa na Imam Ahmad kwa nambari (6597), Abudaud kwa nambari (5079), Tirmidhiy kwa nambari (3529), Nasaai kwa nambari (7699). Shekh Ibnibaz - Allah amrehemu - amesema kuwa orodha (Isnadi) ya wapokezi wake ni sahihi
3 MARA
بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
“Hakuna mja yeyote anayesema mara tatu kila siku asubuhi na kila siku usiku: “Bismillahilladhii Laa Yadhurru Ma’asmihii Shay-un Fil-ardhwi Walaa Fissamaa-i Wahuwassamiiul ‘Aliimu”, (Kwa Jina La Allah ambaye hakuna chochote kinachodhuru pamoja na jina lake si ardhini wala mbinguni. Na yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi), isipokuwa kwamba hakuna chochote kitakachomdhuru”. Hadithi hii ameipokea Imamu Ahmad kwa nambari (10179), Imamu Ibnimaja kwa nambari (3869). Shekh Ibnibaz - Allah amrehema kuwa, amesema Tirmidhiy kwamba “Ni Hadithi sahihi” na ni hivyo alivyosema - Allahu amrehemu.
3 MARA
رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَبِيًّا
“Hakuna mja yeyote Muisilamu ambaye husema mara tatu pindi anapopambazukiwa na pindi anapofikiwa na jioni: “Radhiitu billaahi Rabban, Wabil-islaami Diinan, Wabimuhammaddin – Swallallaahu ‘Alayi Wasallama Nabiyyan” (Nimeridhia kuwa Allah ndiye Mola, na Uislamu ndio dini, na Muhammad SAW ndiye Mtume), ila inakuwa haki kwa Allah kumuridhisha mja huyo Siku ya Qiyama”. Ameipokea Imaam Ahmad kwa nambari (18967), Tirmidhiy kwa nambari (3389) na Ibnimaja kwa nambari (3870). Shekh Ibnibaz - Allah amrehemu - amesema kuwa orodha (Isnadi) ya wapokezi wake ni Hasan (inakubalika).
1 MARA
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ، وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي، وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي
“Allaahumma inniy as-alukal‘aafiyah fid-dun-yaa wal-aakhirah. Allaahumma inni as-alukal‘afwa wal‘aafiyata fii Diiniy wadun-yaaya, wa-ahliy, wamaaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin rau’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni-yadayya, wamin-khalfiy, wa‘an-yamiyniy, wa‘an-shimaaliy, wamin-fawqiy, wa-a’uuwdhu bi’adhwamatika an-ughtaala min-tahtiy”, (Ewe Allaah, hakika nakuomba uzima (utimamu) duniani na Akhera. Ewe Allah, hakika nakuomba msamaha na utimamu katika Dini yangu na dunia yangu, na familia yangu, na mali yangu. Ewe Allah, nisitiri aibu zangu na itulize hofu yangu. Ewe Allah, nihifadhi mbele yangu na nyuma yangu na kulia kwangu na kushoto kwangu na juu yangu. Na naomba kinga kwa utukufu wako nisivamiwe {na adui, maafa, majanga au misiba}). Ameipokea Imamu Ahmad kwa nambari (4785), Abudaudi kwa nambari (5074), Nasai kwa nambari (10401) na Ibnimaja kwa nambari (3871). Imam Hakim amesema kuwa ni Hadithi sahihi.
3 MARA
أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ
“A’uudhu Bikalimaatillaahit-taam-maati Min-Sharri Maakhalaq”, (Naomba hifadhi kwa maneno ya Allah yaliyotimia anilinde dhidi ya shari ya alivyoviumba). Ameipokea Ahmad kwa nambari (7898), na Tirmidhiy kwa nambari (3437) ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abuhuraira – RAA -. Shekh Ibnibaz amesema kuwa Isnadi (orodha) ya wapokezi wake ni Hasan (inakubalika), Allah amrehemu.
1 MARA
أَمْسَيْنَا عَلَى فِطْرَةِ الْإِسْلَامِ، وَكَلِمَةِ الْإِخْلَاصِ، وَدِينِ نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ - صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ - وَمِلَّةِ أَبِينَا إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا, وَمَا كَانَ مِنْ الْمُشْرِكِينَ
“Mtume – SAW - akipambazukiwa alikuwa anasema: “Aswbahnaa ‘Alaa Fitwratil-islaam, Wakalimatil-ikhlaasw, Wadiini Nabiyyinaa Muhammadin – Swallaallahu ‘Alayhi Wasallam -, Wamillati Abiinaa Ibraahim, Haniifan, Wamaa Kaana Minalmushrikiin,” (Tumeingia asubuhi tukiwa katika maumbile ya Kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad Swalla Allahu ‘Alayi Wasallam, na mila (dini) ya baba yetu Ibrahimu iliyo sawa na hakuwa miongoni mwa mwenye kumshirikisha Allah). Imepokewa na Ahmad kwa nambari (15367, 21144). Na akifikiwa na jioni anasema: “Amsaynaa ‘Alaa Fitwratil Islaami…”. Shekh Ibnibaz - Allah amrehemu - amesema kuwa ni Hadithi sahihi.
1 MARA
يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيثُ أَصْلِحْ لِي شَأْنِي كُلَّهُ، وَلَا تَكِلْنِي إِلَى نَفْسِي طَرْفَةَ عَيْنٍ
“Yaa Hayyu Yaa Qayyuum, Birahamtika Astaghiith, Aslih-lii Sha-‘nii Kullah, Walaa Takilnii ilaa Nafsii Twarfat ‘Ain”, (Ewe Uliye hai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba msaada. Nitengenezee mambo yangu yote, wala Usiniachie mambo yangu mwenyewe (pasi na kunisaidia) hata kwa muda (mdogo kama muda) wa kupepesa jicho). Imepokewa na Nasai kwa nambari (10405) na Bazaar (2/282). Ibnihajar na Albaniy wamesema kuwa ni Hadithi Hasan. (Angalia: Nataaijul Afkaar, ukurasa 177, na Silsilatul Ahaadiithisswahiiha 1/449).
7 MARA
حَسْبِيَ الله لاَ إِلهَ إِلاَّ هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرشِ الْعَظِيمِ
“Hasbiyallaahu, Laa ilaaha illa huwa, ‘Alayhi Tawakkaltu Wahuwa Rabbul ‘Arshil ‘Adhwiim. Mwenye kuyasema mara saba, Allah atamtosheleza na (kumuondolea) jambo linalomhuzunisha”, (Allah tu ananitosha. Hakuna apasaye kuabudiwa ila Yeye tu. Yeye nimemtegemea, na Yeye ni Mola wa Arshi Tukufu). Ameipokea Abudaud kwa nambari (5081) ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abudardai – RAA -. Kauli yenye nguvu zaidi ni kwamba Hadithi hii ni “Mawquuf” (Imeishia kuhusishwa na Swahaba tu). Wapokezi wake ni waaminifu, na ina hukumu ya kuhusishwa na Mtume, kama alivyosema Shekh Albaaniy. (Angalia: Silsila 11/449).