languageIcon
search
search
beforeFajronColorIcon / Utangulizi/ ( IDADI YAKE 3 SUNNA )
brightness_1 Mifano ya Ari ya Salaf (Wema Waliotangulia) katika kutenda Suna:

1/ Imamu Muslim katika kitabu chake cha “Sahiih” amepokea Hadithi ya Nuuman bin Salim akinukuu kwa Amri bin Ausi, Allah Awawie radhi, akisema kwamba, amenisimulia Anbasa bin Abisufiaa, kwa kuesema kuwa: Nimemsikia Ummuhabiba akisema: Nimemsikia Mtume (SAW) akisema: “Mwenye kuswali rakaa kumi na mbili kwa usiku na mchana (yaani kwa siku moja), atajengewa nyumba peponi kwa (sababu ya) rakaa hizo”. Hadithi hii imepokelewa na Imamu Muslim, ikiwa na nambari (1727). Na amesema Ummuhabiba: “Sikuziacha (rakaa hizo) tangu nilipozisikia kwa Mtume (SAW)”.  Na Anbasa amesema: “Sikuziacha (rakaa hizo) tangu nizisikie kwa Ummuhabiba.”

Na Amri bin Aus amesema: “Sikuziacha (rakaa hizo) tangu nizisikie kwa Anbasa”.

Na Nuuman bin Salim amesema: “Sikuziacha (rakaa hizo) tangu nizisikie kwa Amri bin Aus”.

2/Hadithi ya Ali, Allah amuwie radhi, : “Kwamba Fatuma alilalamikia hali iliyokuwa ikimsibu katika mkono wake kutokana na jiwe la kusagia nafaka (ili apatiwe mfanyakazi).  Na Mtume, SAW alikuwa amepata mateka. Fatuma alikwenda kwa Mtume lakini hakumkuta. Alikutana na Aisha na kumwambia (shida yake). Mtume –SAW- , alipokuja Aisha alimwabia kuhusiana na kuja kwa Fatma. Mtume –SAW- akaja kwetu, hali ya kuwa tulikuwa tumeshajilaza. Tukataka kuinuka, na Mtume –SAW- akatukataza, na akakaa kati yetu mpaka nikapata ubaridi wa miguu yake katika kifua change. Kisha Mtume akasema: “Je, niwafundishe kilicho bora zaidi kuliko kile mlichokiomba? Mnapotaka kulala mtukuzeni Allah kwa kusema Allahu Akbar mara thalathini na nne, na mtakaseni kwa kusema Sub-haanallaah mara thalathini na tatu, na mhimidini kwa kusema Alhamdu Lillaah mara thalathini na tatu. Kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko (kutafuta) mfanyakazi”. Hadithi hii imepokewa na Bukhaari ikiwa na nambari (3705) na Muslim ikiwa na nambari (2727).

Na katika upokezi mwingine imenukuliwa kwamba, Ali, Allah amuwie radhi, amesema kuwa: “Sikuacha kufanya hayo tangu niyasikie kwa Mtume- SAW-. Aliulizwa: (Hukuacha) Hata katika usiku wa (vita vya) Siffin? Akasema: “Hata katika usiku wa Siffin”.  Hadithi hii imepokewa na Bukhari namba (5362) na Muslim kwa nambari (2727).

Ijulikanavyo ni kuwa usiku wa Siffin ni usiku uliokuwa n vita. Ali, Allah amuwie radhi, alikuwa kiongozi katika vita hivyo. Pamoja na hali hiyo hakuacha Suna hii.

3/ Ibniumar, Allah amuwie radhi, alikuwa anaswalia maiti kisha anaondoka na hamsindikizi kwa kudhani kuwa hiyo ndio Suna kamilifu. Hakuwa akijua fadhila na wema wa kumsindikiza maiti mpaka kuzikwa. Ilipomfikia Hadithi ya Abuhuraira, Allah amuwie radhi, alijuta kwa kuikosa Suna. Tafakari; alifanya nini?!

Ibniumar, Allah amuwie radhi, alitupa chini ya ardhi kwa hasira changarawe iliyokuwa mkononi mwake kisha akasema: “Kwa hakika, tumezikosa kwa uzembe Karati nyingi”. Imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (1324) ,na Muslim ikiwa na nambari (945)

Imamu Annawawi, Allah amrehemu, amesema kuwa: “Ndani ya tukio hilo (la Ibniumar) kunaonekana hali waliyokuwa nayo Swahaba ya kuwa na hamu kubwa ya kufanya ibada pale taarifa inapowafikia na pia kuzijutia ibada zinapowapita hata kama walikuwa hawajui ukubwa wa nafasi yake. Angalia: Alminhaaj (7/15)

brightness_1 Miongoni mwa faida za kufuata Suna:

Ndugu yangu mpendwa, kufuata Suna kuna faida nyingi. Miongoni mwa faida hizo ni:

1/ Kufikia daraja ya kupendwa. Kwa kujiweka karibu na Allah kwa kufanya Suna mja anapata kupendwa na Allah – SWT –.

Ibniqayim, Allah amrehemu, amesema kuwa: “Na Allah hatakupenda isipokuwa tu pale unapokuwa umemfuata kipenzi chake (Mtume) kwa dhahiri na kwa undani, umesadikisha habari zake, umetii amri zake, umeukubali wito wake, umemtanguliza yeye kwa hiari, umeacha sheria za wengine kwa (kutumia) sheria zake, umacha kuwapenda viumbe wengine kwa kumpenda yeye na ukawa umeacha kuwatii wengine kwa kutmii yeye. Kama haitakuwa hivyo, kamwe usisumbuke. Rudi utakako ukatafute nuru, kwani huna kitu chochote”. Angalia kitabu cha Madarijussaalikiin (3/37).

2/ Mja kupata daraja ya kuwa pamoja na Allah (SWT), kwa sababu hiyo Allah humuwezesha mja kufanya mambo ya kheri. Hakitoki kitu katika viungo vyake ila kile kinachomridhisha Allah (SWT), kwa sababu mja anapopata kupendwa na Allah hupata kuwa pamoja naye.

3/ Kujibiwa dua kunakoambatana na kupata kupendwa. Mwenye kujiweka karibu na Allah kwa kufanya Suna atapata kupendwa, na mwenye kupata kupendwa atapata kukubaliwa dua yake.

Ushahidi wa faida hizi tatu ni:

Hadithi ya Abuhuraira, Allah amuwie radhi, aliyesema kwamba, Mtume wa Allah amesema kuwa: “Hakika Allah Amesema: Atakayemfanyia uadui walii wangu (kipenzi change), kwa yakini kabisa nimemtangazia vita, Na mja wangu kwa kitu chochote ninachokipenda zaidi ya vile nilivyomfaradhishia. Na mja wangu ataendelea kujiweka karibu nami kwa kufanya mambo ya Suna mpaka ninakuwa nampenda. Nikimpenda, ninakuwa masikio yake ambayo anasikia kwayo, na macho yake ambayo anaona kwayo, na mkono wake ambao anashika kwao, na mguu wake anaotembelea, Na akiniomba ninampa, na akiniomba kinga ninamlinda.  Na sijapatapo kusita juu ya kitu ninachotaka kukifanya kama kusita kwangu yuu ya nafsi ya muumini; hapendi kufa, nami sipendi kumuudhi”. Hadithi hii imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (6502).

4/ Kuziba upungufu unaopatikana katika kutekeleza Faradhi. Suna huziba yale mapungufu yanayotokea katika (kutenda) Faradhi.

Ushahidi wa hili ni:

Hadithi ya Abuhuraira, Allah amuwie radhi, aliyesema kuwa, nilimsikia Mtume - SAW- akisema kwamba: “Hakika, kitu cha kwanza mja atakachohesabiwa kwacho katika amali zake siku ya Kiyama ni Swala. Swala ikiwa itakuwa iko sawa atakuwa amefaulu na kuokoka. Na swala ikiwa imeharibika atakuwa amepata hasara. Na kama kimepungua kitu chochote katika faradhi zake, Allah atasema: Angalieni: Je, mja wangu ana chochote katika Suna? Kwa Suna hiyo kitakamilishwa kile kilichopungua katika faradhi. Na amali zake zote zilizosalia zitakuwa mfano wa hivyo”.  Hadithi hii imepokewa na Ahmad ikiwa na nambari: (9494) na Abudaudi ikiwa na nambari (864) na Tirmidhi ikiwa na nambari (413).

Ameihakiki Albani (Swahih Aljami 1/405)