languageIcon
search
search
beforeFajronColorIcon Suna za nyakati maalumu/ Alasiri ( IDADI YAKE 2 MILANGO )

1 MARA

brightness_1

أَمْسَيْنَا وَأَمْسَى الْمُلْكُ لِلَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هَذِهِ اللَّيْلَةِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا وَشَرِّ مَا فِيهَا، اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْكَسَلِ، وَالْهَرَمِ، وَسُوءِ الْكِبَرِ، وَفِتْنَةِ الدُّنْيَا، وَعَذَابِ الْقَبْرِ

Amsaynaa wa-amsal-mulku lillaah, walhamdu lillaah. Laa ilaaha illa-llaah, Wahdahuu laa shariyka Lah. Allahumma Innii as-aluka min khayri haadhihil-layla, wakhayri maa fiihaa. Wa-auudhu bika Min-sharrihaa washarri maa fiihaa. Allaahumma innii a’uudhu bika minalkasali, walharami, wasuu-ilkibar, wafitnatid-dun-yaa, wa-adhaabilqabri. (Tupo jioni na ufalme ni wa Allah, na himdi ni za Allah Peke yake, hana mshirika. Ewe Mola wangu, nakuomba kheri zilizomo katika usiku wa leo na kheri za vilivyomo humo. Na ninakuomba kinga dhidi ya shari yake na shari ya vilivyomo humo. Ewe Mola wangu, naomba kinga kwako dhidi ya uvivu, na ukongwe na uzee mbaya, na mtihani wa dunia na adhabu ya kaburini”. Na anapoamka asubuhi aseme kama hivyo: Asbahnaa wa-asbahal-mulku lillaah, walhamdu lillaah. Laa ilaaha illa-llaah, Wahdahuu laa shariyka Lah. Allahumma Innii as-aluka min khayri haadhalyaum, wakhayri maa baadahuu. Wa-auudhu bika Min-sharrihii Min-sharri maa fii Haadhalyaum Washarrimaa baadah. Allaahumma innii a’uudhu bika minalkasali, walharami, wasuu-ilkibar, wafitnatid-dun-yaa, wa-adhaabilqabri. Imepokewa na Muslim kwa nambari (2723).

.......

1 MARA

brightness_1

اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ خَلَقْتَنِي، وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ

Bwana wa Istighfari (Maneno yenye uzito mkubwa katika kumuomba Allah msamaha): “Allahumma Anta Rabbii, Laa Ilaaha illaaa Anta, Khalaqtanii Wa-Anaa ‘Abduka, WaAnaa ‘Alaa ‘Ahdika Wawa’adika Mastata’tu, A’udhu Bika Min-Sharri Maa Swana’atu, Abu’u Laka Bini’imatika Alayya, Wa-abuu-u Laka Bidhanbii, Fagh’fir Lii Fa-innahuu Laa Yaghfirudh-dhhunuuba illaa Anta”. (Bwana wa Istighfari ni kusema: “Ewe Allaah, Wewe ni Mola wangu, hakuna wa kustahiki kuabudiwa ila wewe tu. Umeniumba, na mimi ni mja Wako. Nami niko katika ahadi yako na agano lako kiasi cha uwezo wangu. Naomba kinga kwako dhidi ya ubaya wa niliyoyafanya. Nakiri neema zako kwangu, na nakiri kukukosea, basi naomba unisamehe, kwa sababu hakuna wa kusamehe dhambi ila wewe tu. Amesema Mtume kuwa: (Atakayesema maneno haya mchana akiwa na yakini nayo, na akafa mchana wake huo kabla ya kuingia jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa Peponi. Na atakayesema maneno haya usiku akiwa na yakini nayo na akafa kabla hajafika asubuhi, basi yeye ni miongoni mwa watu wa Peponi)”. Ameipokea Bukhaari, kwa nambari (6306).

.......

1 MARA

brightness_1

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ، وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي، وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي

Allaahumma inniy as-alukal‘aafiyah fid-dun-yaa wal-aakhirah. Allaahumma inni as-alukal‘afwa wal‘aafiyata fii Diiniy wadun-yaaya, wa-ahliy, wamaaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin rau’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni-yadayya, wamin-khalfiy, wa‘an-yamiyniy, wa‘an-shimaaliy, wamin-fawqiy, wa-a’uuwdhu bi’adhwamatika an-ughtaala min-tahtiy”, (Ewe Allaah, hakika nakuomba uzima (utimamu) duniani na Akhera. Ewe Allah, hakika nakuomba msamaha na utimamu katika Dini yangu na dunia yangu, na familia yangu, na mali yangu. Ewe Allah, nisitiri aibu zangu na itulize hofu yangu. Ewe Allah, nihifadhi mbele yangu na nyuma yangu na kulia kwangu na kushoto kwangu na juu yangu. Na naomba kinga kwa utukufu wako nisivamiwe {na adui, maafa, majanga au misiba}). Ameipokea Imamu Ahmad kwa nambari (4785), Abudaudi kwa nambari (5074), Nasai kwa nambari (10401) na Ibnimaja kwa nambari (3871). Imam Hakim amesema kuwa ni Hadithi sahihi.

.......