Imenukuliwa kwa Hudhaifa –Allah Amridhie- akisema kuwa: “Mtume SAW alipokuwa akiamka usiku alikuwa anasugua mdomo wake kwa kutumia mswaki”. Hadithi hii imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (245) na Muslim ikiwa na nambari (255). Na katika mapokezi mengine ya Muslim imenukuliwa kuwa: “Mtume SAW alikuwa anapoamka kufanya Tahajudi (kusali sala za usiku) anasafisha mdomo wake kwa kutumia mswaki”. Hadithi hii ameipokea Muslim ikiwa na nambari (255). Kusafisha: ni kusugua meno kwa upana kwa kutumia mswaki.
Huu ni ule Uradi uliokuja katika Sahih Bukhari kupitia Hadithi ya Hudhaifa, Allah Amridhie, aliyenukuliwa kusema kuwa: “Mtume SAW alikuwa anapotaka kulala anasema: “Kwa jina lako Ewe Mola Wangu ninakufa na ninakuwa hai”. Na anapoamka kutoka usingizini anasema: “Sifa njema ni za Allah Ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na kwake yeye tu ndiko tutakapokusanywa”. Hadithi hii imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (6324) na Muslim kutoka Hadithi ya Albaraa, Allah amridhie, ambayo imepokewa na Muslim ikiwa na nambari (2711).
Na Suna hizi tatu zimekuja katika Hadithi ya Ibniabass, Allah amridhie yeye na baba yake, Hadithi ambayo imepokewa na Bukhari na Muslim kwamba “Yeye (Ibniabbas) alilala siku moja kwa Maimuna mke wa Mtume -SAW- naye ni mama yake mkubwa/mdogo. Nikalala kwa kujiegemeza kwenye mto kwa upana wake, na Mtume –SAW- akalala yeye na mkewe kwa kujiegemeza kwenye mto kwa urefu wake. Mtume akalala mpaka katikati ya usiku, au kabla yake kidogo au baada yake kidogo, Mtume aliamka akaketi akifuta usingizi usoni mwake kwa kutumia mkono wake. Kisha akasoma aya kumi za mwisho katika Sura Aal-imran, Kisha akainuka akachukua kiriba cha maji kilichokuwa kimetundikwa akatawadha vizuri kwa maji yaliyokuwemo humo. Kisha akaanza kuswali”. Hadthi hii imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (183) na Muslim ikiwa na nambari (763).
Na katika mapokezi ya Imamu Muslim yakiwa na nambari (256) imenukuliwa kwamba: “Na Mtume wa Allah –SAW- akasimama wakati wa mwisho wa usiku, kisha akatoka akaangalia mbinguni, kisha akasoma aya hii iliopo mwisho wa Sura Aal-imran.
:{إِنَّ فِي خلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَاخْتِلاَفِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لآيَاتٍ لِّأُوْلِي الألْبَابِ...}[آل عمران190 ]
Kwa hakika, katika umbo la mbingu na ardhi na kupishana kwa usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili…. (Sura Aal-imran: 190).
- akiwa anapangusa usingizi usoni mwake kwa kutumia mkono wake”. Anapangusa macho yake kwa kutumia mkono wake ili apanguse athari ya usingizi.
Na katika mapokezi ya Imamu Muslim kuna ubainifu wa anachokisoma mwenye kutaka kufuata Suna hii. Ataanza kusoma kwanzia kauli ya Allah aliyetukuka: “Kwa hakika katika umbo la mbingu na ardhi na kupishana kwa usiku na mchana…” mpaka mwisho wa Sura Aal-imran.

Ni kutokana na Hadithi ya Abuhuraira –Allah amridhie- aliyenukuu kwamba, Mtume SAW amesema: “Mmoja wenu anapoamka kutoka katika usingizi wake asiingize mkono wake katika chombo mpaka auoshe mara tatu, kwa sababu hajui mahali mkono wake ulipolala”. Hadithi hii imepokewa na Bukhari ikiwa na namba (162) na Muslim ikiwa na namba (278).
Ni kutokana na Hadithi ya Abuhuraira –Allah amridhie- akinukuu kwamba, Mtume SAW amesema: “Mmoja wenu anapoinuka kutoka usingizini mwake asukutue pua mara tatu, kwa sababu shetani analala ndani ya tundu za pua yake”. Hadithi hii imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (3295).