brightness_1
Wakati wa Dhuha ni Suna Mja aswali Swala ya Dhuha.
Na ushahidi wake ni:
a. Hadithi ya Abuhuraira – RAA – amesema aliyenukuliwa kusema kuwa: “Ameniusia rafiki yangu (Swallallaahu ‘alayhi wasallam) mambo matatu: kufunga swaumu siku tatu katika kila mwezi, rakaa mbili za Dhuhaa na niswali Witiri kabla ya kulala”. Na pia Mtume – SAW -alimuusia mambo hayo Abudardai – RAA – (Muslim 722). na Abudhari – RAA – (Nasai – Assunan Alkubraa). Shekh Albani amesema kuwa Hadithi hii ni sahihi.
b. Hadithi ya Abudhari – RAA - akimnukuu Mtume –SAW- kwamba, amesema kuwa: “Panapopambazuka, inakuwepo sadaka katika kila kiungo cha mmoja wenu. Kila Tasbihi (Sub-haanallaah = Ametakasika Allah) ni Sadaka, na kila Tahmidi (Alhamdu Lillaah = Sifa njema ni za Allah) ni sadaka, na kila Tahalili (Laa ilaaha illallaah = Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu) ni sadaka, na kila Takbira (Allaahu Akbar = Allah ni Mkubwa zaidi) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka. Na yote hayo yanatoshelezwa na rakaa mbili anazoswali mtu wakati wa Dhuha”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (720).
Viungo: Ni sehemu ya mwili iliyojigawa.
Na umekuja ufafanuzi katika Sahihi Muslim ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Aisha – RAA – kwamba kila mwanadamu ameumbwa akiwa na viungo mia tatu na sitini, na kwamba mwenye kuleta idadi hii ya sadaka, atakuwa anatembea siku hiyo akiwa ameepushwa na moto wa Jahanamu.