brightness_1
NI KATIKA SUNA KUZUIA MIAYO AU KUFUNIKA MDOMO KWA MKONO.
Na hoja ya hilo ni:
Hadithi ya Abuhuraira- RAA- akimnukuu Mtume –SAW- kwamba, amesema kuwa: “Hakika, Allah anapenda chafya na anachukia miayo. Mtu akipiga chafya akamhimidi Allah, ni haki kwa kila Muisilamu aliyesikia amuombee dua ya “Yarhamukallaah”. Ama miayo, hakika hiyo inatokana na shetani, na kwa sababu hiyo, mtu aizuie kadiri awezavyo. Kama mtu atasema: “haaa”, Shetani humcheka”. Ameipokea Bukhari kwa nambari (2663).
Na kwa mapokezi ya Muslim ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abusaid – RAA - imenukuliwa kwamba, Mtume-SAW- amesema kuwa: “Mmoja wenu anapopiga miayo, aweke mkono wake kwenye mdomo wake, kwa sababu Shetani huingia”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (2995). Kuzuia kupiga miayo kunakuwa kwa kuudhibiti ama kwa kufunga mdomo ili kuzuia usifunuke, au kwa kubananisha meno, au kwa kuweka mkono mdomoni, na mfano wa hivyo.