NI KATIKA SUNA KUZUIA MIAYO AU KUFUNIKA MDOMO KWA MKONO.
Na hoja ya hilo ni:
Hadithi ya Abuhuraira- RAA- akimnukuu Mtume –SAW- kwamba, amesema kuwa: “Hakika, Allah anapenda chafya na anachukia miayo. Mtu akipiga chafya akamhimidi Allah, ni haki kwa kila Muisilamu aliyesikia amuombee dua ya “Yarhamukallaah”.Ama miayo, hakika hiyo inatokana na shetani, na kwa sababu hiyo, mtu aizuie kadiri awezavyo. Kama mtu atasema: “haaa”, Shetani humcheka”.Ameipokea Bukhari kwa nambari (2663).
Na kwa mapokezi ya Muslim ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abusaid – RAA - imenukuliwa kwamba, Mtume-SAW- amesema kuwa: “Mmoja wenu anapopiga miayo, aweke mkono wake kwenye mdomo wake, kwa sababu Shetani huingia”.Imepokewa na Muslim kwa nambari (2995). Kuzuia kupiga miayo kunakuwa kwa kuudhibiti ama kwa kufunga mdomo ili kuzuia usifunuke, au kwa kubananisha meno, au kwa kuweka mkono mdomoni, na mfano wa hivyo.
Na pia iliyo bora kwa mwenye kupiga miayo asitoe sauti yake kwa kupiga miayo
-Na pia iliyo bora kwa mwenye kupiga miayo asitoe sauti yake kwa kupiga miayo, kama kusema (haa), au (aaaah) na mfano wa sauti kama hizo, kwa sababu kufanya hivyo kunapelekea mtu kuchekwa na Shetani.
Na hoja ya hilo ni:
Hadithi ya Abuhuraira -RAA- akimnukulu Mtume –SAW- kwamba, amesema kuwa: “Kupiga miayo kunatokana na shetani. Mmoja wenu anapopiga miayo, ajizuie kadiri awezavyo, kwa sabab anaposema: “Aaah” shetani humcheka”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (3298) na Muslim kwa nambari (2994).
Angalizo:
Baadhi ya watu wamezoea kusema “Auudhu Billaahi Minash-haytwaanirrajiim”= “Naomba hifadhi kwa Allah dhidi ya shetani aliyetengwa” baada ya kupiga miayo. Hakuna hoja juu ya hilo, bali ni kufanya tofauti ya mwongozo wa Mtume-SAW-, kwa sababu mwenye kufanya hivyo atakuwa ameleta uradi ambao hakuufundisha Mtume -SAW- katika pahala hapa.
MAWASILIANO
SISI
TUNAFURAHISHWA KUWASILIANA KWAKO NA SISI NA MASWALI YAKO KWA WAKATI WOWOTE.