brightness_1
NI KATIKA SUNA KUANZA MGUU WA KULIA KATIKA KUVAA VIATU.
Ni katika Suna Muislamu anapotaka kuvaa viatu vyake aanze na mguu wa kulia, na anapotaka kuvivua aanze na mguu wa kushoto.
Na hoja ya hili ni Hadithi ya Abuhuraira –RAA- aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume wa Allah –SAW- amesema kwamba: “Mmoja wenu anapovaa viatu aanze kulia, na anapovua aanze kushoto. Mguu wa kulia uwe wa mwanzo kuvalishwa kiatu na uwe wa mwisho kuvuliwa”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (5856).
Na katika matamshi mengine ya Muslim kuna nukuu kwamba: “Asitembee mmoja wenu akiwa kavaa kiatu kimoja. Yatakikana avae vyote au avivue vyote”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (2097).
Katika Hadithi hizi mbili kuna Suna tatu:
1. Aanze mguu wa kulia wakati wa kuvaa viatu.
2. Aanze mguu wa kushoto wakati wa kuvua viatu.
3. Avae viatu vyote viwili au avue vyote, ili asitembee akiwa kava kiatu kimoja.