languageIcon
search
search
brightness_1 KUTAJA JINA LA ALLAH MWANZO WA KULA.

Imenukuliwa kwa Umar bin Abusalama – RAA – akisema kuwa: “Nilikuwa kijana mdogo chini ya ulezi wa Mtume wa Allah, na mkono wangu ulikuwa ukizungukazunguka hovyo katika sinia (ya chakula). Mtume wa Allah akaniambia: “Ewe kijana! Taja jina la Allaah na kula kwa mkono wako wa kulia, na ule kilicho mbele yako”. Basi huo ukawa ndio mtindo wangu wa kula baadaye.  Imepokewa na Bukhari kwa nambari (5376) na Muslim (2022).

Na mtu akisahau kutaja jina la Allah: Ni Suna aseme pale anapokumbuka; “Bismillaahi Awwalahuu Wa-aakhirah”, ({nakula} Kwa jina Allah Mwanzo wake na mwisho wake).

Kwa mujibu wa Hadithi ya Aisha – RAA – kwamba, Mtume wa Allah–SAW-amesema kuwa: “Anapokula mmoja wenu ataje jina la Allah. Na akisahau kutaja jina la Allah mwanzo wake aseme: “Bismillaahi Awwalahuu Wa-aakhirah”. Imepokewa na Abudaud kwa nambari (3767) na Tirmidhi kwa nambari (1858). Na Shekh Albani amesema kuwa ni Hadithi sahihi, kama ilivyotangulia kuelezwa.

Pia Hadithi hii ni ushahidi kwamba, mwanadamu anatakiwa ale kwa mkono wake wa kulia ili asijifananishe na shetani. Muislamu anapokuwa hajataja jina la Allah, shetani hushirikiana naye katika chakula chake. Na anapokula au kunywa kwa mkono wake wa kushoto, anajifananisha na shetani kwa kufanya hivyo, kwa sababu shetani anakula na kunywa kwa mkono wake wa kushoto.

Na hoja ya hili ni:

Hadithi ya Abdallah bin Umar – RAA – kwamba, Mtume wa Allah–SAW-amesema kuwa: “Asile mmoja wenu kwa mkono wake wa kushoto, wala asinywe kwa mkono huo, kwa sababu Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto na anakunywa kwa mkono huo”.  Na Imam Naafi alikuwa anazidisha: “Wala asipokee (kitu) kwa mkono huo (wa kushoto) na wala asitoe (kitu kumpa mtu) kwa mkono huo (wa kushoto)”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (2020).

Na Shetani hutaka sana kuingia katika majumba ili alale humo na ashirikiane na watu wa majumba hayo chakula na kinywaji.  Imepokewa kwa Jabir bin Abdallah- RAA- kwamba, alimsikia Mtume –SAW-akisema kuwa: “Mtu anapoingia nyumbani kwake au anapokula akamtaja Allah wakati wa kuingia kwake na wakati wa kula kwake, Shetani husema (kuwaambia mashetani wenzake kuwa): “Hmna mahali pa kukaa wala chakula”. Lakini mtu akiingia bila ya kumtaja Allah, Shetani husema (kuwaambia mashetani wenzake kuwa): “Mmepata mahali pa kukaa”. Na Muislamu asipomtaja Allah wakati wa kula, Shetani husema (kuwaambia mashetani wenzake kuwa):  “Mmepata mahali pa kukaa na chakula”.  Imepokewa na Muslim kwa nambari (2018).