languageIcon
search
search
brightness_1 Ni Suna kwa wanaume kuwahi Safu ya kwanza

Ni Suna kwa wanaume kuwahi Safu ya kwanza, kwa Sababu ndio Safu bora zaidi. Na kwa wanawake Safu bora zaidi ni ya mwisho.

Kwa mujibu wa Hadithi ya Abuhuraira – Allah amridhie – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume – SAW – amesema kwamba: Safu bora zaidi ya wanaume ni Safu ya kwanza, na Safu mbaya zaidi ni Safu ya mwisho. Na Safu bora zaidi ya wanawake ni Safu ya mwisho, na Safu mbaya zaidi ya wanawake ni (Safu yao) ya kwanza”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (440). Maana ya Bora zaidi ni kwamba: Ina thawabu na fadhila nyingi sana. Na maana ya mbaya zaidi ni kwamba: Ina thawabu na fadhila chache sana.

Na Hadithi inalenga ni pale wanaume na wanawake watakaposwali pamoja; yaani kwa Jamaa, na hakuna kizuizi kati yao kama vile ukuta na mfano wake. Hapo, itakuwa safu bora ya wanawake ni safu ya mwisho, kwa sababu itakuwa ndio sitara zaidi kwao wasionekane na wanaume. Ama pale penye kizuizui kati ya safu za wanaume na wanawake, kama vile ukuta na mfano wake au kama ilivyo katika misikiti yetu mingi siku hizi ambapo wanawake wametengewa eneo maalumu lenye kujitegemea, katika hali hii safu bora zaidi ya wanawake ni safu ya kwanza, kwa sababu ya kukosekana kwa sababu ya kuwa karibu na wanaume. Hukumu huzunguka kufuata sababu yake kwa kuwepo na kwa kukosekana. Pia ni kwa sababu ya kuwepo kwa Hadithi kadhaa za jumla zinzoelezea ubora wa safu ya kwanza. Baadhi ya Hadithi hizo ni hizi zifuatazo:

Hadithi ya Abuhuraira – Allah amridhie – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume wa Allah –SAW- amesema kwamba: “Lau kama watu wangejua (faida, fadhila na mema) yaliyomo kwenye Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate (njia ya kupata nafasi ya kuwa katika safu ya kwanza) ila kwa kupiga kura, wangepiga kura. Na lau kama wangejua (faida, fadhila na mema) yaliyomo katika kwenda msikitini mapema, wangelishindania. Na lau kama wangelijua (faida, fadhila na mema) yaliyomo ndani ya Swala ya Alfajiri na Swala ya Isha wangeliziendea japo kwa kutambaa”.  Imepokewa na Bukhari kwa nambari (615) na Muslim kwa nambari (437).