languageIcon
search
search
brightness_1 Kufuatisha anavyosema Muadhini.

Ni Suna kwa anayesikia Adhana aseme mfano wa vile anavyosema Muadhini, isipokuwa katika mara mbili za tamko la: “Hayya Alas-swalaa” na “Hayya Alal-falaah”. Hapo atasema: “Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah”.

Kwa mujibu wa Hadithi ya Abdallah bin Amri bin Al-aasw – Allah amridhie yeye na baba yake – aaliyenukuliwa kusema kuwa, alimsikia Mtume –SAW- akisema: “Mnapomsikia Muadhini semeni mfano wa vile anavyosema”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (384). Pia Suna hii ya kufuatisha anavyosema Muadhini imethibiti kwa mujibu wa Hadithi ya Umar bin Alkhattwaab –Allah amridhie – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume –SAW- amesema kwamba: “Muadhini anaposema Allahu Akbar, Allahu Akbar, na mmoja wenu akasema: Allahu Akbar Allahu Akbaru. Kisha (Muadhini) akisema: Ash-hadu Allaa Ilaaha Illallaah, na (mmoja wenu naye) akasema: Ash-hadu Allaa Ilaaha Illallaah”.  Kisha (Muadhini) akisema: “Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullaah”, (Mmoja wenu naye) akasema: “Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullaah”. Kisha (Muadhini) akisema: “Hayya Alas-swalaa” (Mmoja wenu naye) akasema: “Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah”.  Kisha (Muadhini) akisema: “Hayya Alal-falaah”, (Mmoja wenu naye) akasema: “Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah”. Kisha (Muadhini) akisema: “Allahu Akbar Allahu Akbar” (Mmoja wenu naye) akasema: “Allahu Akbar, Allahu Akbar”. Kisha (Muadhini) akisema: Laa Ilaaha Illallaah, (Mmoja wenu naye) Akasema: ‘Laa Ilaaha Illa Allah’ kutoka ndani ya moyo wake ataingia peponi”.  Imepokewa na Muslim kwa nambari (385).

Wakati wa kufuatisha anavyosema Muadhini kwa Swala ya Alfajiri, mwenye kufuatisha Adhana atasema vile asemavyo Muadhini: “Asswalaatu Khairun Minan-nauum”.