Ni Suna kwa anayesikia Adhana aseme mfano wa vile anavyosema Muadhini, isipokuwa katika mara mbili za tamko la: “Hayya Alas-swalaa” na “Hayya Alal-falaah”. Hapo atasema: “Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah”.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abdallah bin Amri bin Al-aasw – Allah amridhie yeye na baba yake – aaliyenukuliwa kusema kuwa, alimsikia Mtume –SAW- akisema: “Mnapomsikia Muadhini semeni mfano wa vile anavyosema”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (384). Pia Suna hii ya kufuatisha anavyosema Muadhini imethibiti kwa mujibu wa Hadithi ya Umar bin Alkhattwaab –Allah amridhie – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume –SAW- amesema kwamba: “Muadhini anaposema Allahu Akbar, Allahu Akbar, na mmoja wenu akasema: Allahu Akbar Allahu Akbaru. Kisha (Muadhini) akisema: Ash-hadu Allaa Ilaaha Illallaah, na (mmoja wenu naye) akasema: Ash-hadu Allaa Ilaaha Illallaah”.Kisha (Muadhini) akisema: “Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullaah”, (Mmoja wenu naye) akasema: “Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullaah”. Kisha (Muadhini) akisema: “Hayya Alas-swalaa” (Mmoja wenu naye) akasema: “Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah”.Kisha (Muadhini) akisema: “Hayya Alal-falaah”, (Mmoja wenu naye) akasema: “Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah”. Kisha (Muadhini) akisema: “Allahu Akbar Allahu Akbar” (Mmoja wenu naye) akasema: “Allahu Akbar, Allahu Akbar”. Kisha (Muadhini) akisema: Laa Ilaaha Illallaah, (Mmoja wenu naye) Akasema: ‘Laa Ilaaha Illa Allah’ kutoka ndani ya moyo wake ataingia peponi”.Imepokewa na Muslim kwa nambari (385).
Wakati wa kufuatisha anavyosema Muadhini kwa Swala ya Alfajiri, mwenye kufuatisha Adhana atasema vile asemavyo Muadhini: “Asswalaatu Khairun Minan-nauum”.
Uradi huu unasomwa baada ya Shahada mbili.
Baada ya Muadhini kusema: “Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullah” yamara ya pili, ni Suna kusoma ule uradi uliokuja katika Hadithi ya Saad – Allah amridhie – akimnukuu Mtume –SAW- kwamba amesema kuwa: “Mwenye kusema anaposikia Muadhini: Ash-hadu Allaa Ilaaha Illallaah Wahdahuu Laa Shariika Lah. Wa-anna Muhammadan Abduhu Warasuuluh, Radhwiitu Billaahi Rabban, Wabi-muhammadin Rasuulaa, Wabil-islaami Diinaa” yakiwa na maana: (Nashuhudia ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah Peke Yake, hana mshirika, na kwamba Muhammad ni Mja wake na Mtume wake. Nimeridhia Allah kuwa Mola wangu, na Muhammad kuwa Mtume), atasemehewa dhambi zake”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (386).
KUMSWALIA MTUME –SAW- BAADA YA ADHAANA.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abdallah Ibniamri – Allah amridhie yeye na baba yake – akinukuliwa kusema kuwa, Mtume wa Allah –SAW- amesema kwamba: “Mkisikia Muadhini semeni kama anavyosema, kisha niswalieni. Atakayeniswalia mara moja Allah atamswalia mara kumi. Kisha niombeeni kwa Allah nipate Wasila (cheo, daraja). Hiyo ni hadhi peponi haistahiki kupewa isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na nataraji mimi niwe (mja) huyo. Atakayeniombea Wasila, uombezi wangu utakuwa halali kwake (atapata uombezi wangu”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (384).
Na namna bora zaidi katika namna za kumswalia Mtume ni: “Swala Ibrahimia”: Allaahumma Swalli Alaa Muhammad, Wa-alaa Aali Muhammad, Kamaa Swallayta Alaa Ibraahiim Wa-alaa Aali Ibraahiim…..”.
KUSOMA DUA ILIYOTHIBITI BAADA YA ADHANA.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Jabir – Allah amridhie – akinukuliwa kusema kuwa, Mtume wa Allah –SAW- amesema kwamba: “Mwenye kusema pindi anaposikia Adhana: “Allaahuma Rabba Haadhihid-daawati-taamma, Wasswalaatilqaa-ima, Aati Muhammadan Alwasiila Walfadhiila, Wab-ath-hu Maqaaman Mahmuudan Alladhii Wa-adtahu”, (Ewe Allah, Bwana wa ulingano (wito) huu uliotimia, na swala iliyo simama, mpe Muhammad Wasila na fadhila, na mfikishe daraja yenye kusifiwa, ambayo umemuahidi, utakuwa halalikwake Uombezi wangu Siku ya Kiyama”. Hadithi imepokewa na Bukhari ikiwa na nambari (614).
DUA BAADA YA ADHANA.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abdallah bin Amri – Allah amridhie yeye na baba yake - : “Kwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Allah, hakika Waadhiini wanatushinda kwa fadhila. Mtume – SAW – akasema: “Sema kama (Waadhini) wanavyosema, na ukimaliza omba utapewa”.Imepokewa na Abudaud kwa nambari (524). Ibnihajar (Nataa-ijul-afkaar 1/367) pia Albaani (Sahiihulkalimit-twayyib, ukurasa 73) wametaja kuwa ni Hadithi Hasan.
Pia kwa mujibu wa Hadithi ya Anas – Allah amridhie – aliyenukuu kwamba, Mtume – SAW – amesema kuwa: “Dua kati ya Adhana na Iqama hairejeshwi (haikataliwi)”. Hadithi hii imepokewa na Annasai kwa nambari (9895) na Ibnikhuzaima (2/221/425) ameitaja kuwa ni sahihi (1/221/425).
MAWASILIANO
SISI
TUNAFURAHISHWA KUWASILIANA KWAKO NA SISI NA MASWALI YAKO KWA WAKATI WOWOTE.