brightness_1
Kuswali Rakaa mbili kabla ya Magharibi.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abdallah ibn Mughaffal Almuzani – RAA - akimnukuu Mtume – SAW – kwamba, amesema kuwa: “Swalini kabla ya swala ya Magharibi”-, na mara ya tatu akasema: “kwa anayetaka, kwa kuchelea watu wasiifanye kuwa ni Suna”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (1183).
- Na vilevile ni suna kuswali Rakaa mbili kati ya kila Adhana na Ikama.
Ni sawa kwamba hizi Rakaa mbili ni zile za Ratibu (za kabla na za baada), kama suna ya Alfajiri na Adhuhuri au la. Kwa kuswali kwake Suna Ratibu, kwa hakika inatosheleza na hakuna haja ya kuswali Rakaa hizi mbili (za kati ya kila Adhana na Ikama). Mtu kama amekaa msikitini kisha Muadhini akaadhini kwa ajili ya swala ya Alasiri au Ishaa, ni Suna asimame na kuswali Rakaa mbili.
Na ushahidi wa hili ni:
Hadithi ya Abdallah bin Mughaffal Almuzani – RAA – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume – SAW – amesema kwamba: “Kati ya kila Adhana mbili (Adhana na Ikama) kuna Swala”. Mtume alisema hayo mara tatu. Alisema katika mara ya tatu: “Kwa anayetaka”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (624) na Muslim (838).
Hakuna shaka kwamba, Rakaa mbili za kabla ya Magharibi au kati ya Adhana na Ikama hazijatiliwa mkazo sana kama zilivyotiliwa mkazo Suna za Ratibu. Kwa hakika, huwa zinaachwa mara nyingine. Ndio akasema Mtume – SAW – katika mara ya tatu kwamba: “Kwa anayetaka”; kwa kuchelea watu kuifanya kuwa ni Suna (iliyotiliwa mkazo sana).