Ni katika Suna kuwazuia watoto (wasitoke majumbani) mwanzo wa magharibi
Na katika kufanya taratibu hizi mbili kuna kinga dhidi ya Mashetani na Majini. Katika kuwazuia watoto (wasitoke nje) mwanzo wa wakati wa magharibi ni kuwalinda dhidi ya mashetani ambao husambaa katika wakati huo, na katika kufunga milango wakati huo na kutaja jina la Allah-aliyetukuka – kuna kinga pia dhidi ya mashetani na majini.Watoto wengi na nyumba nyingi mashetani wamejipenyeza kwao na kuingia katika wakati huu. Ni ukubwa ulioje wa ulinzi wa dini ya Kiislamu kwa watoto wetu na nyumba zetu!
Na hoja ya hili ni:
Hadithi ya Jabir bin Abdallah - RAA – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume – SAW – amesema kwamba: “Liingiapo giza la usiku wazuieni watoto wenu kutokatoka (majumbani), kwa sababu mashetani wanasambaa nyakati hizo. Likishapita saa moja ya usiku waacheni. Na fungeni milangeni na tajeni jina la Allah (mnapoifunga), kwa sababu shetani hafungui mlango uliofungwa”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (3304) na Muslim kwa nambari (2012). Giza la usiku ni: Kuingia kwa usiku baada ya jua kuzama.
Kuzuia watoto na kufunga milango mwanzo wa magharibi, ni katika hali ya kupendekezwa. Angalia: Fat-wa za Kamati ya Kudumu (26/317).
Ni katika Suna kufunga milango mwanzo wa magharibi, na kutaja jina la Allah –aliyetukuka
Na katika kufanya taratibu hizi mbili kuna kinga dhidi ya Mashetani na Majini. Katika kuwazuia watoto (wasitoke nje) mwanzo wa wakati wa magharibi ni kuwalinda dhidi ya mashetani ambao husambaa katika wakati huo, na katika kufunga milango wakati huo na kutaja jina la Allah-aliyetukuka – kuna kinga pia dhidi ya mashetani na majini. Watoto wengi na nyumba nyingi mashetani wamejipenyeza kwao na kuingia katika wakati huu. Ni ukubwa ulioje wa ulinzi wa dini ya Kiislamu kwa watoto wetu na nyumba zetu!
Na hoja ya hili ni:
Hadithi ya Jabir bin Abdallah - RAA – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume – SAW – amesema kwamba: “Liingiapo giza la usiku wazuieni watoto wenu kutokatoka (majumbani), kwa sababu mashetani wanasambaa nyakati hizo. Likishapita saa moja ya usiku waacheni. Na fungeni milangeni na tajeni jina la Allah (mnapoifunga), kwa sababu shetani hafungui mlango uliofungwa”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (3304) na Muslim kwa nambari (2012). Giza la usiku ni: Kuingia kwa usiku baada ya jua kuzama.
Kuzuia watoto na kufunga milango mwanzo wa magharibi, ni katika hali ya kupendekezwa. Angalia: Fat-wa za Kamati ya Kudumu (26/317).
Kuswali Rakaa mbili kabla ya Magharibi.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abdallah ibn Mughaffal Almuzani – RAA - akimnukuu Mtume – SAW – kwamba, amesema kuwa: “Swalini kabla ya swala ya Magharibi”-, na mara ya tatu akasema: “kwa anayetaka, kwa kuchelea watu wasiifanye kuwa ni Suna”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (1183).
- Na vilevile ni suna kuswali Rakaa mbili kati ya kila Adhana na Ikama.
Ni sawa kwamba hizi Rakaa mbili ni zile za Ratibu (za kabla na za baada), kama suna ya Alfajiri na Adhuhuri au la. Kwa kuswali kwake Suna Ratibu, kwa hakika inatosheleza na hakuna haja ya kuswali Rakaa hizi mbili (za kati ya kila Adhana na Ikama). Mtu kama amekaa msikitini kisha Muadhini akaadhini kwa ajili ya swala ya Alasiri au Ishaa, ni Suna asimame na kuswali Rakaa mbili.
Na ushahidi wa hili ni:
Hadithi ya Abdallah bin Mughaffal Almuzani – RAA – aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume – SAW – amesema kwamba: “Kati ya kila Adhana mbili (Adhana na Ikama) kuna Swala”. Mtume alisema hayo mara tatu. Alisema katika mara ya tatu: “Kwa anayetaka”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (624) na Muslim (838).
Hakuna shaka kwamba, Rakaa mbili za kabla ya Magharibi au kati ya Adhana na Ikama hazijatiliwa mkazo sana kama zilivyotiliwa mkazo Suna za Ratibu. Kwa hakika, huwa zinaachwa mara nyingine. Ndio akasema Mtume – SAW – katika mara ya tatu kwamba: “Kwa anayetaka”; kwa kuchelea watu kuifanya kuwa ni Suna (iliyotiliwa mkazo sana).
Ni Makuruhu (haipendezi) kulala kabla ya Isha.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abubarza Al-aslami – RAA - aliyenukuliwa kusema kuwa, Mtume “Alikuwa anapendelea kuchelewesha Isha. Amesema: Na alikuwa anachukia kulala kabla ya Isha, na mazungumzo baada yake”. Ameipokea Bukhari namba (599), na Muslim kwa namba (647).
Na sababu ya kuchukia kulala wakati wa Magharibi; yaani kabla ya Isha ni kwa sababu kulala kwake kunaweza kuwa sababu ya kupitwa na Swala ya Isha.
MAWASILIANO
SISI
TUNAFURAHISHWA KUWASILIANA KWAKO NA SISI NA MASWALI YAKO KWA WAKATI WOWOTE.