brightness_1
Wakati wa joto kali. Ni Suna kuchelewesha Swala yua Adhuhri Mpaka joto lipungue.
Na ushahidi wa hilo ni:
Hadithi ya Abuhuraira – RAA - ambayo imehusishwa na Mtume kwamba: “Jua linapokuwa kali sana ngojeni hadi lipoe ndipo mswali, kwa sababu ukali wa joto unatokana na mtokoto wa Jahanamu”.
Kutokota kwa Jahanam: Ni kuchemka kwake na kusambaa kwa miali na sauti yake. Ameipokea Bukhari kwa nambari (533,534), na Muslim kwa nambari (615).
Shekhe wetu Ibniuthaimini - Allah amrehemu – amesema kuwa: “Tukikadiria, kwa mfano, kuwa jua katika siku za joto linapinduka saa sita, na Alasiri inakuwa takribani saa kumi na nusu, basi Ibraad (kuliacha joto lipoe) itakuwa hadi takribani saa kumi”. Angalia: Almumti’u (2/104).
Na Ibradi ni kwa watu wote; anayeswali kwa jamaa na mwenye kuswali peke yake, katika kauli iliyo sahihi. Na hii ndiyo kauli aliyoichagua Shekhe wetu Ibniuthaimini - Allah amrehemu. Kwa kauli hiyo, wanawake pia wanaingia, na maana hiyo, ni Suna kwao kusubiri hadi joto lipoe wakati wa jua kali, kwa mujibu maana jumla ya Hadithi ya Abuhuraira –RAA-.