Imetangulia katika maelezo juu ya Suna za Ratibu (swala za suna zilizowekewa muda maalumu) kwamba sheria imeweka Suna kuswali rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na rakaa mbili baada ya Adhuhuri, kama inavyolitolea ushahidi hilo Hadithi ya Aisha, Ummuhabiba na Ibniumar, Allah awawie radhi wote.
Ni katika Suna kurefusha Rakaa ya kwanza ya Swala ya Adhuhuri.
Kwa mujibu wa Hadithi ya Abusaid Alkhudriy – RAA – aliyenukuliwa kusema kuwa: “Hakika, ilikuwa swala ya Adhuhuri inakimiwa, kisha mwenye kwenda anakwenda mpaka Baqii na kukidhi haja yake, kisha anatawadha na kurudi na ilhali Mtume – SAW - akiwa bado yupo katika Rakaa ya kwanza, kwa namna alivyokuwa akiirefusha”. Ameipokea Muslim kwa nambari (454).
Kutokana na hayo, ni katika Suna kwa imamu kurefusha rakaa ya kwanza ya swala ya Adhuhuri, na vilevile mwenye kuswali peke yake, na pia mwanamke katika swala yake ya Adhuhuri. Na hii ni katika Sunnah ambazo zimetoweka (zimekufa). Tunaomba Allah – aliyetukuka - atuwezeshe kutekeleza Suna kwa namna iliyo kamilifu, na kuiwekea maanani.
Wakati wa joto kali. Ni Suna kuchelewesha Swala yua Adhuhri Mpaka joto lipungue.
Na ushahidi wa hilo ni:
Hadithi ya Abuhuraira – RAA - ambayo imehusishwa na Mtume kwamba: “Jua linapokuwa kali sana ngojeni hadi lipoe ndipo mswali, kwa sababu ukali wa joto unatokana na mtokoto wa Jahanamu”.
Kutokota kwa Jahanam: Ni kuchemka kwake na kusambaa kwa miali na sauti yake. Ameipokea Bukhari kwa nambari (533,534), na Muslim kwa nambari (615).
Shekhe wetu Ibniuthaimini - Allah amrehemu – amesema kuwa: “Tukikadiria, kwa mfano, kuwa jua katika siku za joto linapinduka saa sita, na Alasiri inakuwa takribani saa kumi na nusu, basi Ibraad (kuliacha joto lipoe) itakuwa hadi takribani saa kumi”.Angalia:Almumti’u (2/104).
Na Ibradi ni kwa watu wote; anayeswali kwa jamaa na mwenye kuswali peke yake, katika kauli iliyo sahihi. Na hii ndiyo kauli aliyoichagua Shekhe wetu Ibniuthaimini - Allah amrehemu. Kwa kauli hiyo, wanawake pia wanaingia, na maana hiyo, ni Suna kwao kusubiri hadi joto lipoe wakati wa jua kali, kwa mujibu maana jumla ya Hadithi ya Abuhuraira –RAA-.
MAWASILIANO
SISI
TUNAFURAHISHWA KUWASILIANA KWAKO NA SISI NA MASWALI YAKO KWA WAKATI WOWOTE.