languageIcon
search
search
NYIRADI ZA MCHANA NA USIKU NYIRADI ZA MCHANA NA USIKU ( IDADI YAKE 4 MILANGO )

1 MARA

brightness_1

اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَنْ ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

Ni katika Suna kusoma Aaya Kursi wakati wa kulala, kwa sababu ndani yake kuna kinga dhidi ya Shetani mpaka kunapopambazuka.

Na ushahidi wa hili ni: Kisa cha Abuhuraira –RAA- na mtu aliyekuwa akiiba Zaka. Amesema Abu Hurara –RAA- kuwa: “Na Mtume – SAW- akaniambia kuwa: “Amefanya nini mateka wako (uliyemkamata kwa wizi) usiku wa jana?”. Nikamwambia: “Alidai kuwa atanifundisha maneno ambayo Allah ataninufaisha kwayo, na kwa hiyo, nikamwachia”. Mtume akasema: “Ni yapi maneno hayo?”. Nikamwambia: Ameniambia: “Utakapoingia kitandani kwako (kwa ajili ya kulala), soma Aya Kursi (Allaahu Laa ilaaha illaa Huwal-Hayyul-Qayyuum) kuanzia mwanzo wake hadi uikamilishe”, na (Mwizi) aliendelea kuniambia kuwa: “(Kwa kusoma Aya hiyo) Utaendelea kuwa katika ulizi wa Allah na kamwe Shetani hatakusogelea mpaka asubuhi”.  Na (Swahaba) walikuwa na ari sana ya kujali mambo ya kheri. Hapo, Mtume – SAW - akaniambia: “Amekwambia ukweli japokuwa yeye ni muongo, Je, unamjua ewe Abuhurara uliyekuwa ukizungumza naye tangu siku tatu?” Nikamwambia: “Hapana, ewe Mtume wa Allah -SAW-. Mtume akasema: “Huyo ni Shetani”.  Imesimuliwa na Bukhari kwa nambari (2311) na ameiunganisha Imamu Nasai katika Assunan Alkubraa kwa nambari (10795).

 

.......

1 MARA

brightness_1

اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ وَرَبَّ الأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ، فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى، وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ وَالْفُرْقَانِ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ ، وَأَنْتَ الآخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ، اقْضِعَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْرِ

Allaahumma, Rabbas-Samaawaatis-Sab-I, Warabbal-Ardhwi, Warabbal-‘Arshil-‘Adhwiim, Rabbanaa Warabba Kulli Shai-in, Faaliqal-habbi Wan-nnawaa, Wamunzilat-tauraati Wal-injiil,  Walfurqaan. A’uwdhu Bika, Min-sharri Kulli Shay-in Anta Aakhidhunbinaaswiyatih. Allaahumma, Antal-Awwalu, Falaysa Qablaka Shay-un, Wa-antal-aakhiru, Falaysa Ba’-Daka Shay-un, Wa-antadhw-Dhwaahiru, Falaysa Fawqaka Shay-un, Wa-antalbaatwinu, Falaysa Duunaka Shay-un. Iqdhwi‘Annad-dayna, Wa-agh-ninaa Minal-faqri”, (Ewe Allah, Mola wa mbingu saba na Mola wa ardhi, na Mola wa Arshi Tukufu, Mola wetu na Mola wa kila kitu, Mpasuaji wa mbegu na kokwa, na Aliyeiteremsha Tawrati na Injili na Qur-ani. Naomba kinga kwako dhidi ya shari ya kila kitu wewe ndiye Mwenye kukidhibiti. Ewe Allah, wewe ndiye wa Mwanzo hakuna kitu kabla yako, na wa Mwisho hakuna kitu baada yako, na Uliye juu hakuna kitu juu yako, na Uliye karibu, hakuna kitu kilicho karibu kuliko wewe. Nilipie madeni na niepushe na ufukara).  Imepokewa na Muslim (2713).

.......

100 MARA

brightness_1

سبحان الله (33)، الحمد لله (33)، الله أكبر (34) م

Ni katika Suna mtu anapotaka kulala aseme “Sub-haanallaah” mara thalathini na tatu, na “Alhamdulillaah” mara thalathini na tatu, na “Allaahu Akbar” mara thalathini na nne. Jambo hili lina fadhila kubwa sana, nayo ni kuwa linaupa mwili nguvu katika siku yake.

Na ushahidi wa hili ni Hadithi ya Ali – RAA – “Kwamba, Fatma alilalamika juu ya ugumu aliokuwa akiupata katika mkono wake kutokana na jiwe la kusagia nafaka, na Mtume – SAW – alikuwa amepata mateka. Fatma akaondoka kwenda kwa Mtume – SAW – (ili apewe mfanyakazi wa nyumbani), lakini hakumkuta, na akakutana na Aisha na kumwambia (shida yake ya kuomba kupewa mfanyakazi). Mtume – SAW – alipokuja, Aisha alimwabia kuhusu kuja kwa Fatma. Mtume –SAW- akaja kwetu, tukiwa tumeshajilaza. Tukataka kuinuka, na Mtume –SAW- akatuambia “Tulieni hivyo hivyo mlivyo”, na akakaa kati yetu mpaka nikapata ubaridi wa miguu yake katika kifua change. Kisha akasema: “Je, mnaonaje nikufundisheni kilicho bora zaidi kuliko kile mlichokiomba? Mnapoenda kulala mtakaseni Allah mara thalathini na tatu, na Mhimidini mara thalathini na tatu na mtukuzeni mara thalathini na nne. Hayo ni bora zaidi kwenu kuliko (kutafuta) mfanyakazi”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (3705) na Muslim kwa nambari (2727).

Na katika mapokezi mengine imenukuliwa kwamba Ali –RAA- alisema kuwa: “Sikuyaacha maneno hayo tangu nilipoyasikia kwa Mtume –SAW-. Akaulizwa: Hata katika usiku wa (vita vya) Siffin? Akajibu: Hata katika usiku wa (vita vya) Siffin”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (5362) na Muslim kwa nambari (2727).

 

.......

1 MARA

brightness_1

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْلَمْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ، وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ، وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ. لاَ مَلْجَأَ وَلاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إِلَيْكَ، آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ، وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ

Allaahumma, innii aslamtu nafsiy ilayka, wafawwadhwtu amriy ilayka, wa wajjahtu waj-hiya ilayka, wa-alja-tu dhwahriy ilayka, raghbatan warahbatan ilayka. Laa malja-a walaa man-jaa Minka illaa ilayka. Aamantu Bikitaabikal-ladhiy Anzalta wabinabiyyikal-ladhiy Arsalta”, (Ewe Allah, nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia wewe mambo yangu, na nimeuelekeza uso wangu kwako, na nimeugemeza mgongo wangu kwako (nakutegemea wewe katika kusimamia mambo yangu kamwa mwanadamu anavyotegemea mgongo katika kusimama), kwa matajarajio (ya kupata rehema zako) na kwa kukuogopa (adhabu yako). Hakuna sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako tu. Nimekiamini kitabu chako ulichokiteremsha na Nabii wako uliyemtuma). Ameipokea Bukhari kwa nambari (247) na Muslim kwa nambari (2710). Katika mwisho wa Hadithi Mtume – SAA – amesema kuwa: “Na yafanye maneno hayo yawe maneno yako ya mwisho. Ukifariki usiku huo utafariki ukiwa katika maumbile ya asili (ya Tawhiid= kumwamini Allah tu). Na katika upokezi wa Muslim imenukuliwa kwamba Mtume amesema: “Na ikiwa utapambazukiwa, utapambazukiwa ukiwa katika kheri”.

Na katika Hadithi hii kuna ubainifu wa Suna nyingine. Suna hii ni kwamba, mtu anatakiwa afanye uradi huu uwe maneno yake ya mwisho anayoyatamka kabla hajalala. Pia kuna tuzo kubwa, nayo ni kwamba lau kama mtu atakadiriwa kufa usiku huo, atakuwa katika wale walokufa katika maumbile ya asili; yaani atakufa akiwa katika Suna katika mila ya Ibrahimu –AS-. Na akipambazukiwa atakuwa amepambazukiwa juu ya kheri katika riziki yake, na kazi yake. Uradi huo ni tamko lenye kukusanya yote yaliotangulia na mengine, na Allah ni Mjuzi zaidi.

.......

1 MARA

brightness_1

اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ

Na miongoni mwa mambo yanayopasa kutolewa angalizo ni: Uradi mkubwa ambao ni sababu ya kupata fadhila kubwa. Allah Aliye Mtukufu amejigamba kwa uradi huo uliokuja katika Sahihi Bukhari, ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Shadad bin Aus – RAA – akimnukuu Mtume –SAW- kwamba amesema kuwa: “Bwana wa kuomba maghfira (Dua kubwa) ni kusema, Allaahumma, anta Rabbiy, laa ilaaha illaa Anta. Khalaqtaniy wa-ana ‘abduka. Wa ana ‘alaa ‘ahdika wa wa’adika mastatwa’atu. A’uudhu bika min-sharri maa swana’atu. Abuu-u laka bini’imatika ‘alayya, wa abu-u laka bidhan-biy, faghfirliy, fa-innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta”, (Ewe Allah, wewe ni Mola wangu, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa wewe tu. Umeniumba na mimi ni mja wako, na mimi nimo katika kutekeleza maamrisho yako kadiri niwezavyo. Ninaomba kinga kwako dhidi ya kila shari niliyoitenda, Ninakiri neema zako kwangu, na ninakiri kukukosea.  Kwa hivyo, nisamehe kwa sababu hakuna mwenye kusamehe madhambi isipokuwa wewe tu. Akasema: Atakayesema hayo wakati wa mchana akiwa na yakini nayo, na akafa siku hiyo kabla ya usiku kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi. Na atakayesema hayo wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, na akafa kabla ya asubuhi kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi”. Ameipokea Bukhari kwa nambari (6306).

.......