Kwa mujibu wa Hadithi ya Thabit Albunani akimnukuu Anas –RAA- kwamba amesema kuwa: “Hakika, mimi siwezi kuacha kukuswalisheni kama nilivyomuona Mtume –SAW- akituswalisha”. Akasema: “Anas –RAA-alikuwa anafanya kitu ambacho sikuoneni nyinyi mkikifanya. Ainuapo kichwa chake kutoka katika kurukuu alikuwa anasimama wima mpaka msemaji anaweza kusema kuwa, labda amesahau. Na ainuapo kichwa chake kutoka katika kusujudu anakaa mpaka msemaji anaweza kusema kuwa, labda amesahau”. Imepokewa na Bukhari kwa nambari (821) na Muslim kwa nambari (472).
Kuleta aina tofauti za matamshi ya “Rabbanaa, Walakal-hamdu” kati ya matamshi yafuatayo:
a. “AllaahummaRabbanaa walakal-hamdu”,(Ewe Allah Mola wetu, na ni zako wewe tu sifa njema).Imepokewa na Bukhari kwa nambari (795) ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abuhuraira- RAA-.
b. “AllaahummaRabbanaa Lakal Hamdu”, (Ewe Allah Mola wetu, ni zako wewe tu sifa njema). Imepokewa na Bukhari kwa nambari (796) na Muslim kwa nambari (404) ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abuhraira –RAA-.
c. “Rabbanaa walakal Hamdu”, (Ewe Mola wetu, na ni zako wewe tu sifa njema). Imepokewa na Bukhari kwa nambari (799) na Muslim kwa nambari (411) ikiwa ni sehemu ya Hadith ya Aisha –RAA-.
d. “Rabbanaa Lakalhamdu”, (Ewe Mola wetu, ni zako wewe tu sifa njema). Imepokewa na Bukhari kwa nambari (722) ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abuhuraira –RAA-.
Ni Suna mara alete aina hii na mara nyingine alete aina nyingine.
Baada ya kunyanyuka kutoka katika Rukuu, ni suna kuleta nyiradi zilizothibiti.
Na miongoni mwa nyiradi ambazo sheria imeziweka baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu ni hizi zifuatazo:
a. “Rabbanaa Lakalhamdu, Mil-ussamaawaati Wal-ardhi, Wamil-u Maashi-ita Min Shai-in Baadu, Ahluth-thanaa-i Walmajdi, Ahaqqu Maaqaalal-bdu, Wakullunaa Laka Abdu, Allaahumma Laa Maania Limaa Aatwaita, Walaa Muutwiya Limaa Manaata. Wala Yan-fau Dhaljaddi Minkaljaddu”,(Ewe Allah Mola wetu, ni zako wewe tu sifa njema, ujazo wa mbingu na ardhi, na ujazo wa chochote ulichotaka (kuumba) baadaye. Ewe Mwenye kustahiki sifa na utukufu. La kweli kabisa alilolisema mja, na sisi sote kwako ni waja, ni kwamba: Hakuna wa kuzuia ulichotoa, na hakuna wa kutoa ulichozuia. Na wala mali haziwezi kumnufaisha tajiri kwako). Imepokewa na Muslim kwa nambari (477), na Muslim ikiwa ni sehemu ya Hadithi ya Abusaid-RAA.
b. “Alhamdulillahi, Hamdan Kathiiran, Twayyiban, Mubaarakan Fiihi”, (Sifa njema ni za Allah, sifa nyingi, nzuri, zenye Baraka). Amesema Mtume-SAW- juu ya matamshi haya kwamba: “Nimewaona Malaika kumi na mbili wakishindana nani atakayeiyapeleka juu”. Imepokewa na Muslim kwa nambari (600) na Bukhari kwa nambari (799).
c. “Allahumma, Twah-hirnii, Bith-thalji, Walbaradi, Walmaa-ilbaarid, Allahumma, Twah-hirnii, Minadh-dhunuubi, Walkhatwaayaa, Kamaa Yunaqqath-thaubul Abyadhu, Minal Wasakh’’, (Ewe Allah Mola wangu, Nisafishe kwa theluji na barafu aa maji baridi. Ewe Allah Mola wangu, Nisafishe niondokane na madhambi na makosa kama vile inavyotakaswa nguo nyeupe iondokane na uchafu).Imepokewa na Muslim kwa nambari (476).
Na Muislamu akileta nyiradi hizi ataweza kurefusha nguzo hii.
MAWASILIANO
SISI
TUNAFURAHISHWA KUWASILIANA KWAKO NA SISI NA MASWALI YAKO KWA WAKATI WOWOTE.